Kwa nini ganda la kobe lina nyufa
Lewis Mutugi
Lewis Mutugi

Hapo zamani palikuwa na Mzee Kobe. Aliishi peke yake kwa nyumba ya matope. Siku mmoja alihisi njaa sana na kwa vile alipenda mambe aliamua kwenda kuyatafuta. Jua nalo lilikuwa limewaka kama moto.

1

Ulikuwa msimu wa kiangazi hivyo basi, chakula kilikuwa adimu. Alijikokota pole pole akielekea msituni.

2

Alipokuwa njiani aliona miti mitatu. Mti mmoja ulikuwa wa maembe yaliyokuwa yameiva. Alipoyaona alitabasamu. Papo hapo aliamua kuyaendea.

3

Aliwaza na kuwazua jinsi atakavyo upanda ule mti kuyachuna maembe kwa sababu yalikuwa juu sana.

4

Alijitia moyo na kuyaendea yale maembe kwa mshindo. Halikuwa jambo rahisi kamwe kwa Mzee Kobe kuukwea ule mti.

5

Baada ya kupanda juu alishikilia kwa tawi. Kobe huyu alikuwa na uzito kupita kiasi. Tawi hilo halikustahimili uzito wake.

6

Lile tawi lilivunjika na Mzee Kobe akaanguka chini kwa mshindo pu!. Ganda lake lililokuwa nyororo likapasuka na kupata nyufa.

7

Kobe alijutia kitendo chake cha kupanda mti. Alirudi nyumbani akiwa na njaa na kuudhika kwa kuwa urembo wake umefika mwisho.

8
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Kwa nini ganda la kobe lina nyufa
Author - Lewis Mutugi
Illustration - Lewis Mutugi
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs