Binti ya Mfalme na Chura
Nelly Kawira
Elvis Mwiti

Hapo kale paliishi binti ya mfalme na chura.
Binti huyu alimchukia chura sana.

1

Mfalme alimpa bintiye kila kitu ambacho alitaka. Alichoka kucheza na vitu ambavyo babake alikuwa amempa kisha akaamua kumuomba ampe mpira wa dhahabu.

2

Siku moja Binti huyo alienda kucheza karibu na mto. Alikuwa akirusha mpira huo juu kisha anaunasa.

3

Alirusha mpira juu tena ukaanguka mtoni kabla ya kuunasa. Alianza kulalamika huku akilia kwa machungu. Punde si punde, yule chura alitokea mara tu aliposikia sauti ya Binti.

4

Binti alimweleza kilichotokea. Kwa huruma, chura alitumbukia ndani ya mto na kuutafuta mpira. Baada ya muda mchache, alitoka na ule mpira wa dhahabu. Kwa furaha tele Binti alinyakua mpira na kutimua mbio hadi ikuluni.

5

Bila kusita chura alimwandama unyo unyo hadi ikulu na kubisha mlango. Binti alipofungua mlango na kumuona chura, alimshika na kumtupa nje.

6

Chura aligeuka na kuwa mwana wa mfalme. Binti alipigwa na butwaa alipoona hivyo.

7

Binti alimuomba msamaha kwa kumtenda vibaya. Baada ya hapo akamtambulisha kwa babake. Mfalme alifurahi kuwaona pamoja.

8

Mfalme aliwaandalia harusi nzuri ambapo walibadilishana viapo vyao na baadaye wakaishi kwa furaha.

9
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Binti ya Mfalme na Chura
Author - Nelly Kawira
Illustration - Elvis Mwiti
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs