

Tita na toto ni pacha.Wao hupenda kufanya vitu pamoja. Wako darasa la tano .Siku Moja walipo kuwa wametoka shuleni walikutana na mzee mmoja akiwa amelewa sana .Yule mzee alikuwa anaonekana mtu mwenye pesa.
Wewe ni nani? Toto aliuliza kwa uoga.Yule Mzee akacheka kwa sauti huku akijingamba.'Hebu muone ulivyo nenepa utadhani nitangi la maji' Toto akasema kwa sauti. 'Unawezaje akumusema Babu yenu hivyo?' Mzee akasema.Tita na Toto walishanga Sana
Toto akapaza sauti huku akisema 'Wewe ni tapeli,unatudanganya, wewe ni muongo, hiyo haiwezi kuwa kweli.' Yule mzee akasema kwa unyenyekevu. "Basi kama huniamini twende Moja kwa Moja Hadi mnapoishi."
"Wewe umelewa,haujui unacho kiongea" Toto akasema. Mara waliongozana kwa pamoja kuelekea nyumbani.Walipofika kule nyumbani,mama yao alipomwona yule mzee,alimkimblia mbio na kusema," karibu baba yangu karibu tena."
Mama Yao akawaambia "huyu ni babu wenu". Toto na Tito waliposikia hivyo walimwomba msamaha yule mzee.Babu akawasamehe,wakaingia nyumbani,wakala. Usiku huyo babu yao aliwaambia hadithi za zamani, wakafurahi.

