

Asha Juma ,mtoto wa Mzee Juma Ali na mke wake Pili Mbwana.Asha ni kiziwi na hutumia sana alama za ishara.
Watoto wenzake wengi huwa hawajui alama za ishara hivyo hata kusoma kwake ni kwa shida sana.
Asha anajihisi upweke sana. Hana marafiki wengi na hata mawasiliano inakuwa ngumu mno.
Watoto wengine humuonesha dharau na kumkatisha tamaa ya maisha .Hata majirani na ndugu pia humuonyesha dharau, sio vizuri kabisa.Jambo linalomuumiza kama binadamu
Mama yake anamuandaa kwaajili ya kwenda shule.Leo amepata nafasi ya kushiriki michezo shuleni na hajakubali kuachwa nyuma.
Duu ! leo Asha amecheza mpira vizuri mpaka watu wameshangaa kipaji chake.''Kumbe Asha ana kipaji ameweza kushindana na hata wanaume.'' watoto wenzake wanasema.
Tusamehe sana Asha , kweli tulikudharau na kukataa urafiki na wewe.Tumekuumiza , tunaomba tuwe marafiki .Asha anakubali na wanakumbatiana.
Asha amepata marafiki wengi sasa na amepata mwalimu kwaajili ya wanafunzi viziwi na anafanya vizuri darasani .Anacheza mpira kwenye timu ya wasichana MILEMBWE
Ndoto ya Asha ni kuwa mchezaji mpira bora katika timu ya taifa ya wanawake.Sasa shuleni kwao wamekuja wanafunzi wengine watano viziwi na wote husoma na kucheza pamoja.
Watu hudhani kuwa ukiwa mlemavu huwezi kufanya kitu .Si kweli, ulemavu usikufanye ukate tamaa ya maisha .Pia tusidharau watu , kwani hujafa hujaumbika.
Ulemavu unaweza kumpata mtu yoyote , wakati wowote .Lakini wewe utabaki kuwa wa thamani sana , thamani yako haifananishiwi na chochote duniani.Pambania ndoto zako.
Leo nimekuwa mchezaji mpira bora , nimekuwa mwenye thamani zaidi .Mimi nimeweza , hata wewe unaweza .Sote tunaweza

