

Mimi naitwa Amina. Wazazi wangu walinipa sehemu ndogo ya shamba ambayo nilitumia kupanda maua.
Kila asubuhi natembelea shamba langu kumwagilia maua maji na kutoa magugu.
Siku moja niliamua kwenda kumtembelea nyanyangu. Nilienda shambani kuchuma maua. Nilitaka kumpa shada la maua kutoka bustani yangu. Nilipokuwa nachuna maua, niligundua mawingu yameanza kubadilika kana kwamba mvua ingenyesha.
Baada ya umeme kupiga, papo hapo palitokea mngurumo na radi ikawa ishara tosha kuwa mvua kubwa ingenyesha.
Wazo lilinijia nikimbie nyumbani kabla mvua kunipata. Mara baada ya wazo hilo, kulianza kunyesha na maji ikalowa kwenye ardhi. Niliteleza na kuanguka chini pu!
Nilipoinuka, nilihisi uchungu mwingi. Niligundua kuwa nimeumia mgongo na paji la uso. Mara familia yangu ilinipeleka hospitalini.
Pale hospitalini madaktari walinitibu na kuniitunza vyema. Familia yangu pia walinitembelea na kuniiletea maua kutoka kwenye shamba langu ili kunitia moyo niweze kupata nafuu haraka.
Baada ya kukaa hospitalini wiki nzima nilipata nafuu. Daktari aliniruhusu kutoka hospitalini. Wazazi wangu walipokuja kunichukua, muuguzi alinipa dawa ninywe nyumbani. Nilifurahi sana kurudi kwetu.

