Mkulima bora
Rumba Bro
Isaac Okwir

Hapo zamani za kale katika kijiji cha Sirimon paliishi mkulima mmoja aliyeitwa Mzee Tobi na mkewe Maria. Walikuwa na shamba lao ambalo walitumia kupanda mahindi na mimea mingineo.

1

Siku moja Mzee Tobi alirauka machweo kabla ya Shetani kulivaa kanzu lake nyeusi tititi kama makaa kuelekea shambani. Mkewe alimtayarishia chakula cha mchana na kumpelekea shambani. Alimpata mumewe akipalilia mahindi kwa bidii.

2

Baada ya kula chakula chake cha mchana aliendelea kulima shamba. Safari hii tu alikuwa na nguvu zaidi. Kwa minajili ya shibe, jasho lilimtiririka usoni kama maji.

3

Bibi yake alizidi kumkalisha mumewe shambani huku wakipiga gumzo za maneno ya hapa na pale mara kwa mara. Rafikiye Boxy alitilia maanani mazungumzo yao kana kwamba alielewa yalikuwa yanahusu nini.

4

Ghafla, palitokea Sungura aliyekuja kushambulia mimea yao. Mzee Tobi kumuona alimrushia lile jembe kwa hasira huku Boxy akimkimbiza kwa kasi.

5

Walighadhabika sana kuona jembe lao limevunjika vipande vipande baada ya kumurushia yule Sungura.

6

Mioyo yao ikijawa na fadhaa wakijiuliza watafanya nini. Hapo ndipo mke wake alipendekeza aende nyumbani alete jembe lingine ili mumewe akamilishe kazi aliyokusudia kuifanya hiyo siku.

7

Bila kupoteza muda, mkewe alitimua mbio nyumbani na kumletea mumewe jembe lingine ili aendelee kulima shamba. Wote wawili walijawa na furaha kwamba kazi ilikamilika.

8
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Mkulima bora
Author - Rumba Bro
Illustration - Isaac Okwir
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs