

Hapo zamani za kale paliishi sungura na fisi. Walikuwa wamependana kama Chanda na Pete. Siku moja sungura akamwambia fisi waende wakachune maembe.
Sungura Mjanja akamwambia fisi, "tutafunga macho yetu, yule atachuna maembe mengi yameiva atakuwa Mshindi." Bila Shaka, fisi alikubali wachune maembe. Sungura na ujanja wake akafungua macho kidogo ili aone maembe yaliyokuwa yameiva.
Sungura akachuna mazuri akiwekea fisi maembe mbichi, huku akijiwekea yameiva na kidogo mabichi. Muda ulipowadia wa kushuka alishuka akiwa wa Kwanza. Fisi akamuuliza, "Kwa nini maembe yangu hayajaiva ilhali yako yameiva?"
Fisi alisirika Sana. Alimkimbiza sungura Kwa Kasi. Punde si punde, Sungura akaona pango chini ya mti.
Sungura alipokuwa anaingia Kwa shimo, fisi alimshika mguu wa kulia. Naye sungura akamwambia amuachilie mguu wa kulia amshike mguu wa kushoto. Fisi aliposhika mguu wa kushoto, sungura aliingia ndani ya lile pango zaidi.
Mwewe akaja na kumuuliza fisi nini anakodolea macho ndani ya Pango. Fisi akamwambia mwewe amkalishe sungura asitoke ndani ya pango ili aweze kwendea shoka nyumbani. Fisi alipoenda sungura aliitoka pangoni na kumdanganya mwewe.
Sungura alimwabia mwewe Kuna nyama walipewa Kwa sherehe Fulani, na fisi ana mpango wa kulia peke yake. Alimwambia mwewe amuache aende ili amletee nyama wale pamoja. Bila kusita, mwewe alijawa na furaha tele kisha akampa sungura ruhusa.
Mara hio, sungura alitimua mbio akielekea chini ya ule mti ambapo walikuwa wameacha maembe yao.Kwa haraka sungura aliyatia maembe yaliyokuwa yameiva Kwa gunia na kutimua mbio.
Tangu siku hiyo urafiki wa Sungura na Fisi ulifika kituo.

