SOMOE MTUNDU
MORIC ZAMBUKE
Brian Wambi

Hapo zamani za kale palikuwa na mabinti wawili ndugu,Walioitwa SOMOE na BUNGA

1

Bunga alikuwa mkubwa kwa SOMOE,BUNGA alikuwa mtoto mtiifu,Lakini SOMOE alikuwa mtundu Sana..

2

Siku moja walikuwa njiani kurudi nyumbani,wakitokea kwa shangazi yao,walipita njia fupi ya porini..

3

Kwakuwa SOMOE ni mtundu sana,njiani alipanda mti mrefu sana.

4

BUNGA Alimsihi SOMOE asipande mti huo mrefu Lakini alichelewa..

5

Baadae SOMOE alipotaka kushuka alishindwa,Alioogopa aliona chini ni MBALI Sana

6

SOMOE alikaa hapo kwa muda mrefu akiwa analia,Hadi walipokuja wazazi wake,Wakamsaidia kushuka

7

Wazazi walimuonya SOMOE kuacha utundu, Wakimwambia Angeliwa na DUBU siku hiyo..

8

Toka siku hiyo SOMOE akawa mtoto mzuri,akawasikiliza wazazi akaacha UTUNDU...

9
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
SOMOE MTUNDU
Author - MORIC ZAMBUKE
Illustration - Brian Wambi
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs