

Ng'ombe, ng'ombe, nipe maziwa!
Moo moo, omba vizuri!
Ng'ombe, Ng'ombe, tafadhali naomba maziwa.
Haya hapa tayari kwa kunywa.
Asante rafiki!
Kuku, Kuku, nipe mayai!
Kokoo, kokoo, omba vizuri!
Kuku, Kuku, tafadhali naomba mayai.
Sawa Atu, chukua mawili!
Asante rafiki!
Chura, Chura, nifundishe kuruka!
Hapana Atu, omba vizuri.
Chura, Chura, tafadhali naomba unifundishe kuruka?
Sawa Atu, turuke pamoja!
Asante rafiki!
Kipepeo, Kipepeo, nisukume kwa nyuma!
Hapana Atu, omba vizuri!
Kipepeo, Kipepeo, tafadhali naomba unisukume kwa nyuma.
Sawa Atu, furahia bembea! Asante rafiki!
Baiskeli, Baiskeli nipe lifti.
Ngrii, ngrii, omba vizuri!
Baiskeli, Baiskeli tafadhali naomba lifti.
Sawa Atu, panda juu.
Asante rafiki.
Paka, Paka, fukuza panya!
Nyau, nyau, omba vizuri!
Paka, Paka, tafadhali naomba umfukuze panya?
Panya, ondoka, Atu anakuogopa!
Asante rafiki!
Mbuzi, Mbuzi, nipeleke nyumbani!
Meh, meh, omba vizuri.
Mbuzi, Mbuzi, tafadhali unipeleke nyumbani?
Sawa Atu, panda mgongoni.
Asante rafiki!
Atu, Atu, tupeleke Lala Land.
Hapana, rafiki, omba vizuri!
Atu, Atu, tafadhali tunaomba utupeleke Lala Land.
Sawa nitawapeleka! Tucheze siku nzima na tusubiri usiku.
Tukifumba macho upinde utakuja kutupeleka Lala Land.
Angalieni, unatokea! Twende Lala Land!

