Ziara ya Mombasa
Naomi Karimi
Abraham Muzee

Kim na binamu yake Caro, wilipanga kwenda Mombasa kumtembelea shangazi yao. Siku ya safari waliamka mapema kujitayalisha.

Walikuwa wandamane na mjomba wao Sifa. Saa mbili kasororobo, mlango ukabishwa. Kim alikimbia kuufungua.

1

"Mjomba Sifa, karibu sana! Tuko tayari," Kim alimwamkua.

"Samahani sitaweza kufunga Safari leo.Nina Jambo la tharura sana.Nitawapeleka katika kituo cha Gari moshi harafu shangazi wenu atawasubili stasheni Mombasa.

2

Walifika katika stesheni ya Gari moshi ya Nairobi na kuabili gari hilo.Baada ya muda mfupi,garimoshi liliondoka kwenye stesheni kwa mwendo wa Kasi.wakampungia mkono mjomba wao Tobiko wakiwa na furaha tele.

3

Baada ya muda wa masaa matatu hivi safarini muhudumu aliwapakulia chakula cha mchana.Ni raha iliyoje kuandaliwa chakula ndani ya garimoshi.Kim na Caro walicheza mchezo wa kadi Safarini huku wakipanga maeneo watakayozulu walifika Mombasa.

4

Walifika Mombasa jioni.Shangazi yao alikuwa amewasubili karibu na lango lakuondoka stesheni.Shangazi aliwapeleka nyumbani kwake.
Kesho yake Baada ya kuoga waliondoka kuzulu Fort Jesus ambapo waliona ngome na vitu za zamani sana.

5

Waliona sanamu za waswahili na kisima cha zamani kilichotumiwa na wareno.Pia waliona chumba mahalumu kilichotumika kama ngeleza na wakoloni.

6

Ilipofika saa saba mchana walienda kula chamcha kisha wakaelekea Bamburi kwa matembezi ya msituni.Msituni walimuona kobe mkubwa sana mwenye miaka zaidi ya mia moja.wakapigwa picha naye.Pia waliwaona pundamilia sungura na twiga.

7
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Ziara ya Mombasa
Author - Naomi Karimi
Illustration - Abraham Muzee, Rob Owen
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs