Konokono
Njeri Wachira
Kamau Njuguna

Nilinunua masanduku ya mbao na kuyaweka kando ya nyumba yangu.

1

Nikamwaga mchanga wenye rutuba ndani yake. Nikapanda mbegu tofauti: za sukuma wiki, kabeji, mchicha, dania na stroberi.

2

Kila asubuhi niliamka alfajiri na mapema kunyunyizia maji kwa mfereji.

3

Baada ya wiki moja nilipiga tabasamu kubwa nilipoona mimea ilikuwa imechipuka.

4

Baada ya wiki mbili nilipigwa na mshangao nilipoenda kunyunyizia maji. Niliona mimea ikiwa na mashimo makubwa kwenye majani yake. Nilijua kuna adui aliyekuwa akila mimea yangu.

5

Usiku mmoja nilitoka nje na kurunzi yangu na kuangaliaangalia karibu na mimea. Niliona konokono na koa uchi chungu nzima. Wengine walikuwa juu ya mimea yangu niliyoidhamini.

6

Nikajaribu maganda ya mayai. Lakini wapi! Mimea iliendelea kuharibiwa.

7

Nilijaribu tembe za dukani. Lakini wapi! Konokono waliendelea kuangamiza mimea yangu.

8

Niliamua kuwawinda konokono mimi mwenyewe.
Nilitoka nje usiku mmoja kama nimejihami kwa kurunzi, mkebe na glovu mkononi.

9

Nikaangalia juu ya mimea, kando yake na chini yake. Kila nilipomwona konokono nilimweka ndani ya mfuko.

10

Baada ya kuzunguka nilipata kama kilo moja ya konokono. Nifanye nini nao? Niwachemshe wawe kitoweo au niwatupe pipani?

11

Kila usiku nilitoka kwenda kuwinda konokono na baada ya wiki mbili niliona mimea yangu inanawiri tena.
Kumbe kuwasaka konokono kulisaidia!

12
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Konokono
Author - Njeri Wachira
Illustration - Kamau Njuguna, Njeri Wachira
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs