

Hapo zamani, paliishi paka kwa jina Jaga. Jaga alikuwa wa kipekee, wakutamanika, na mwenye rangi ya kuvutia wengi. Alikuwa na afia nzuri kabisa na alikuwa akila chakula kitamu na kupendeza pale mtaani kama mkate,keki,nyama na kunywa mazi
Jaga aliishi katika duka la mzee Taji.Hili ni duka lililokuwa kubwa kuliko maduka mengine katika mtaa ule na iliuzwa karibu bidhaa zote ambazo hutumika nyumbani. Watu waliishi kujaa pale wakinunua unga,nafaka,mafuta,sukari na zinginezo
Jaga alipenda sana maisha ya mtaani. Watoto walicheza naye Kila siku.wengine walimpa keki ili kumvutia kwao.Jinzi siku ziliendelea kusonga ndivio Jaga aliendelea kuwa mkunbwa na angelida lile duka la bwana Taji na kuzuia panya kuhari vyakul
la. Siku moja duka la mzee Taji Lilivamiwa na wezi na walichukuwa vitu vingi sana. Watu walipofika kusaidia wezi walikuwa wameenda zao tayari na ilikuwa Jambo mbaya sana la kuhuzunisha.
Mzee Taji aliamua kurudi kijijini na kuanzisha kilimo. Hivyo basi lazima Jaga angemfuata bwana Taji kijijini na wote wawili waliona wazo nzuri. Hivyo basi aliamua kufuga ng'ombe,mbuzi,mbwa na kuku.
Siku za mwazoni maisha ya kijijini yalikuwa kama Yale ya mtaani. Mzee Taji aliweza kumnunulia Jaga chakula kitamu. Siku zilivyosonga bwana Taji alianza kuwa na kazi nyingi. Jaga hangeweza kumfuata Kila mahali na alianza kuaachwa nyumbani.
Jioni bwana Taji angerudi akiwa amechoka kutoka shambani na hangeweza kununua vitamu vya kumpa Jaga.Jaga alianza kujifunza maisha mapya. Akaaza kuwinda ili kupata chakula kizuri. Siku moja alikula kuku,na jioni ililpofika Bwana Taji
akamkosa. Alipopitapita Shambani aliona manyoya ya kuku. Bwana Taji alimpa mkate na maziwa akanywa maziwa kidogo tu.Jaga aliwala kuku wote pale nyumbani. Mbwa wa bwana Taji hakupendezwa na tabiya ya Jaga. Baada ya siku kadthaa kupita bwana
Taji alijua kuwa Jaga ndiye amekula kuku wote. Alikasirika sana kumtukuza.Kutoka siku Ile mbwa wa bwana Taji akawa anamtukuza Jaga. Taji alimsamehe Jaga na kumkaribisha tena lakini chuki kati ya mbwa na Jaga haikuisha hadi siku ya leo

