

Tembo Mdogo alikuwa akitembea porini na mamake na dadake mkubwa. Walikuwa wakiimba kwa sauti na kurusha vumbi.
Kwa bahati mbaya, Tembo Mdogo akajikwaa kwenye jiwe na hakuweza kutembea tena. Alibaki nyuma.
Mama na dada waliendelea bila kujua kama Tembo Mdogo alikuwa amebaki nyuma.
Tembo Mdogo hakujua pa kuenda. Alianza kulia kwa uoga.
Kwa bahati nzuri Panda alikuwa ndani ya majani karibu na mahali ambako Tembo Mdogo alikuwa ameketi chini.
Panda alimsongea akamwambia, "Nifuate. Mahali hapa kuna wanyama wengine ambao wanaweza kukuumiza."
Tembo Mdogo hakusita kukubali kwa sababu hakuwa na mahali pengine pa kuenda. Vilevile kijiji chake kilikuwa mbali.
Walipofika katika kijiji cha Panda, kila mnyama alionyesha uso tofauti. Baadhi ya wanyama walimpenda Tembo Mdogo. Wengine walikasirika na wengine wakaogopa. Hawakujua jinsi mfalme wao Simba angeamua.
Kwa kweli Simba hakukubali Tembo Mdogo abaki katika Kijiji kile. Alisema, "Atakayepinga uamuzi wangu, atafukuzwa pomoja na Tembo Mdogo. Ufalme wangu si wa watu wa nje ila ni wa vizazi vya hapa.
Simba alimwambia Tembo Mdogo, "Nenda mbali au niivunje mifupa yako mara mia."
Tembo Mdogo alishtuka akakosa la kusema. Akaamua kuenda. Lakini, rafiki yake Panda akaona hawezi kumuacha aende peke yake.
Kwa ajili ya upendo aliokuwa nao kwa Tembo Mdogo, Panda aliacha kila kitu na kumrudisha nyumbani.
Tembo Mdogo alifurahi sana hata akambeba mgongoni.

